Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imetakiwa kutatua malalamiko ya upatikanaji wa baadhi ya dawa na vipimo kwa wananchi wenye bima ya afya.Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa kikao na Menejimenti ya Mfuko huo katika ofisi ndogo za wizara zilizopo jijini, Dar es Salaam.
“Kumekuwepo na malalamiko ya upatikanaji wa baadhi ya dawa na vipimo kwa watu wenye kadi za bima pia ucheleweshaji wa malipo ya watoa huduma za afya” Alisema Waziri Ummy.Aidha, Waziri Ummy ameutaka mfuko huo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko huo pamoja na mafao yanayotolewa katika vifurushi vya bima ya afya.“Tatueni malalamiko yote kwa wakati ili wananchi wafurahie vifurushi vyote watakavyojiunga navyo”.Alisisitiza Waziri Ummy.
Kikao hicho pia kiliangalia mwenendo wa utoaji wa huduma za bima za afya zinazotolewa na mfuko huo ambapo kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NHIF, Benard Konga, Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, na Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi Tirioni 11.4 baada ya kushinda mashauri mbalimbali yaliyoendeshwa katika Mahakama mbalimbali ndani na nje ya nchi.Hayo yamezungumzwa mapema leo na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Mhe. Gabriel Malata alipokuwa akipokea msaada wa kompyuta mpakato tano zenye thamani ya shilingi milioni 7.5 zilizotolewa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Mhe. Malata ameeleza kuwa kiasi hicho cha fedha kimeokolewa katika mwaka wa fedha 2019/2020 kufuatia utendaji mzuri wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ambao umepelekea kushinda mashauri mengi yaliyofunguliwa dhidi ya Serikali.Kiongozi huyo aliongeza kuwa fedha hizo zilizookolewa na Serikali zitasaidia katika kuboresha miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kama vile ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), ununuzi wa ndege na meli kubwa za abiria na mizigo katika kuhakikisha tunafikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.Amesema kuwa kompyuta hizo zimekuja muda muafaka kwani zitawawezesha watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu Mkuu wa Serikali kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kwa haraka zaidi hatua itakayosaidia kuongeza ufanisi zaidi katika majukumu yao.Aidha, Naibu Wakili Mkuu ameongeza kuwa kompyuta hizo zitakuwa msaada mkubwa kwa Ofisi yake kwa kuzingatia ukweli kuwa mwaka huu tunaenda kwenye zoezi la uchaguzi hivyo itawawezesha watumishi wake hususani mawakili katika kutekeleza majukumu ya usimamizi wa mashauri.“Mwaka huu tuna jukumu la uchaguzi na uchaguzi huwa unapelekea kuibuka kwa mashauri mengi yanayofunguliwa kwa ajili ya kupinga matokeo ya uchaguzi”, alisema Mhe. Malata.Naye Bw. Muungano Saguya ambaye ni Meneja Huduma kwa Jamii katika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) alisema kuwa wameamua kutoa msaada huo ili kuwasaidia watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha zaidi hatua itakayopelekea kuendelea kuokoa fedha nyingi ambazo zingeweza kupotea kutokana na upungufu wa vitendea kazi ofisini hapa.Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ilianzishwa feburuari 12 mwaka 2018 kwa tangazo la serikali Na. 50 ikiwa na lengo la kuratibu, kusimamia na kuendesha mashauri yote ya madai pamoja na Katiba, Uchaguzi na haki za binadamu yanayofunguliwa dhidi ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Beki wa Liverpool Joel Matip baada ya kufanyiwa vipimo vya kina sasa imethibitika atakosa game zote za Liverpool zilizosalia 2019/20, Matip aliumia mguu wakati wa game ya Liverpool dhidi ya Everton.
CAF watangaza kuwa sababu ya Corona michuano ya AFCON 2021 iliyokuwa ifanyike Cameroon sasa imesogezwa mbele hadi January 2022.
Na Amiri Kilagalila, Njombe.
Wasaidizi wa kisheria nchini wameelezwa kuzingatia maadili katika utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wahitaji ili waweze kupata nafuu na haki inayohitajika kwa mujibu wa sheri.Wito umetolewa na katibu mkuu wa wizara ya katiba na sheria Prof.Sifuni Mchome wakati akizindua kamati ya uratibu wa shughuli za msaada wa kisheria mkoa wa Njombe.
“Katika kazi ni wajibu kuhakikisha maadili yanazingatiwa,maadili katika maeneo mbali mbali,maadili katika ushauri,kupeleka kesi mahakamani na maadili katika mahusiano yetu na watu ambao tunawahudumia,na mtoa msaada wa kisheria hawezia akawa mchonganishi”alisema Prof.Sifuni MchomeAidha Mchome amesema lengo mojawapo la serikali kuwa na wasaidizi wa msaada wa kisheria ni kusaidia katika utetuzi wa migogoro inayojitokeza katika jamii pamoja na kuhakikisha uwepo wa utawala bora.
Naye mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka ameiomba wizara ya katiba na sheria kuongeza nguvu katika kuzisimamia asasi zinazotoa elimu kutokana na uwepo wa asasai zinazofanya kazi isiyokuwa na afya kwa taifa.“Kwa muda mrefu huko nyuma asasi hizi zingine zilikuwa zikifanya kazi ambazo hazina afya kwa ustawi wa nchi na wengine wamekuwa ni madalali wa kusimamia maslai ya nchi zingine za ughaibuni”alisema Ole SendekaKaimu aifisa maendeleo ya jamii mkoa wa Njombe Farahani Kanyenda,amesema wasaidizi na watoa huduma za msaada wa kisheria wamekuwa na msaada mkubwa kwa jamii na kuwezesha idadi ya watu waliopata huduma ya msaada wa kisheria kwa kipindi cha Julai 2019 hadi Mei 20 kufika 8282 kwa upande wa madai,19 kwa upande wa Jinai,26 kwa upande wa matunzo huku watoto waliopata msaada wa kisheria wakiwa 42.Erasto Mkiwa ni mratibu wa shirika la PAD na Geofrey Kaduma ni mkurugenzi wa kituo cha msaada wa sheria Njombe,wanasema licha ya uwepo wa changamoto katika shughuli zao lakini wanaamini kamati iliyoundwa itasaidia kuwafikia zaidi wananchi wenye migogoro mbali mbali.“Kwa kupitia kamati hii itatusaidi kuwafikia zaidi wananchi kwasababu ni sehemu mojawapo ya kurahisisha mawasiliano na kupitia wadau tuliopo ni rahisi kuelewa wapi kuna tatizo”Alisema Erasto Mkiwa
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuwafukuza kazi wafanyakazi wa shirika hilo wanaowatoza fedha na wanaochelewesha zoezi Kutoa nembo ya ubora kwa bidhaa zinazotengenezwa kwenye Viwanda vidogo nchini.Waziri Bashungwa ametoa maelekezo hayo leo 30 juni 2020 alipofanya ziara mkoani Simiyu na kutembelea kiwanda cha Usindikani wa Viazi lishe kilichopo wilaya ya Maswa kinachojulikana kwa jina la Ng’hami Industries Company Ltd.
Bashungwa amefikia maamuzi hayo baada ya kufika kiwandani hapo na kukagua bidhaa za kiwanda hicho ambayo ni unga wa viazi lishe na kugundua hazina nembo ya ubora ya TBS, ambayo changamoto hiyo imesababiswa na wafanyakazi wa shirika la TBS kwa kuwaomba fedha kwa ajiri ya kupewa nembo ya ubora pia kuchewesha kwa zaidi ya miezi saba bila kupewa majibu au nembo ya ubora.Waziri Bashungwa baada ya kuona changamoto hiyo alimpigia simu Mkurugenzi Mkuu wa TBS na DKt. Yusuph Ngenya na kumuelekeza kuwafukuza kazi wafanyakazi wake wanaokwenda kinyume na maagizo ambayo amekuwa akiyatoa mara kwa mara ya kutowachelewesha wafanyabiasha kwa sababu ambazo sio za msingi zinazosababisha bidhaa kutopewa nembo za ubora kwa wakati ambazo zinasababisha mazingira ya Rushwa na usumbufu kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali.Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho Bw. Ntobi Rufunga ameeleza kuwa barua ya kuomba nembo ya ubora ilipelekwa TBS tangu mwezi 11, 2019 lakini mpaka sasa hajapewa majibu yoyote na baada ya kuchukuliwa kwa sampuli ya bidhaa hiyo wameombwa kutoa kiasi cha Tsh. 520,000/= ili wapewe nembo ya ubora ambayo ni kinyume na sheria na mashariti ya shirika hilo.Aidha Bw. Ntobi amesema kuwa Kiwanda hicho mpaka sasa kinazalisha unga wa viazi lishe wa aina mbili ambao ni Unga wa kupika uji kwa ajiri ya matumizi ya rika zote pia Unga wa kutengeneza keki, mikate na andazi.
Yanga yafanikiwa kutinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) baada ya kuipiga Kagera Sugar bao 2-1 katika dimba la Taifa jijini Dar Salaam.Magoli ya Yanga yalifungwa na Molinga dakika ya 52, Kaseke dakika ya 76 kwa mkwaju wa penati na lile la Kagera lilifungwa na Awesu dakika ya 20.
FT: Yanga SC 2-1 Kagera Sugar.
Chenza ni tunda jamii ya chungwa. Licha ya kuwa maeneo mengi yanayostawishwa machungwa, machenza nayo hupatikana lakini si mengi kama machungwa.
Kama mara nyingi ninavyozungumza katika mada zangu mbalimbali kuwa ukimwuliza mtu kwanini una kula chenza atakuambia kwa kuwa ni tunda tamu lakini hawezi kukuambia faida zilizomo ndani ya tunda husika.Ila siku ya leo nitakueleza japo kwa uchache faida zitokanazo na chenza kama ifutavyo;1. Tunda hili ni tamu lina faida nyingi sana katika mwili wa binadamu ikiwemo kuongeza vitamin C,2. Pia linazuia kuvuja damu katika fizi kwa watu wenye matatizo ya kutokwa na damu katika fizi za meno yao.3. Vilevile tunda hili lina imarisha mifupa, linaongeza nguvu katika miusuri nakuondoa maumivu ya viungo.4. Pia linaondoa baridi yabisi, linaondoa viuvimbe chini ya tumbo, linasaidia kuondoa mawe katika figo na kibofu, linatibu unene na mirija ya damu na kutibu udhaifu wa macho.Mara nyingi watalamu wa afya wanashauri kula tunda lenyewe lililowiva tu kwa sababu hili ndilo limesheeni wingi wa faida lukuki kama ambavyo tumeeleza hapo juu.
Kupitia safu yetu ya mahusiano, leo nimekuletea makala maalum hasa kwa wanawake kutokana na malalamiko ya wanawake wengi kuwapoteza waume zao. Kilio chao kikubwa ni kukimbiwa na wanaume au kuachwa.Leo anakuwa na mwanaume huyu, baada ya muda mfupi kunatokea chokochoko, mwanaume anatimka zake.
Jamaa anamkimbia na kwenda kuanzisha uhusiano mwingine. Baada ya kukimbiwa, mwanamke hakati tamaa. Anaanzisha uhusiano mwingine, ndani ya muda mfupi tu, anaambulia maumivu tena. Anabaki kujilaumu. Hajui chanzo cha yeyekukimbiwa.Matokeo ya hili, mwanamke anapoteza uelekeo. Kila mwanaume anayekutana naye anamkimbia. Mwisho wa siku anajikuta umri umeenda. Kuolewa inakuwa ni ndoto. Anaanza kulazimisha kusaka mtoto ili angalau na yeye aitwe mama.Wanaume wengi hujikuta wakiwaacha wapenzi wao kwa sababu ya tabia fulani ambazo wakati mwingine huanza taratibu na baadaye huwa kikwazo kikubwa.Ili kuweza kuepukana na tatizo hili ni vyema tukaangalia vitu ambavyo wanaume wamekuwa hawavipendi kutoka kwa wanawake ili kuweza kujua nini cha kufanya kuhakikisha unamweka mwanaume karibu, asikuache.1. Chokochoko/Maneno Maneno Wanaume wengi huwa hawapendi chokochoko. Hawapendi mwanamke ambaye yeye kila wakati ni kuanzisha chokochoko ambazo zinazalisha ugomvi. Wanaume wengi hawapendi mabishano. Hawapendi ugomvi hivyo mwanamke anapokuwa hodari wa kuleta chokochoko, huepukwa.Ni vyema basi mwanamke akachunga kauli. Akawa si mtu wa kuchimbachimba vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Asiwe na kisirani. Kinywa chake kitawaliwe na maneno matamu, yatakayomtia moyo mpenzi wake, yatakayomfariji na yatakayomfanya apende kuzungumza naye.Mara nyingi mwanaume akiona mke au mpenziwe ni mtu wa kupenda chokochoko, mara nyingi humuepuka. Anajitahidi kadiri ya uwezo wake kukaa naye mbali. Ataona ni bora achelewe kurudi nyumbani akakutane na marafiki baa, wapige stori ili muda uende na akirudi nyumbani asiwe na muda wa kuzungumza na mwenzi wake, yeye ni kula na kulala.2. Kutoridhika Wanaume wengi wanachukia kuwa na wanawake wasioridhika. Baadhi ya wanawake hata uwape nini huwa hawaridhiki. Wanawasumbua wapenzi wao kwamba hawawatimizii mahitaji. Mwanaume anajitoa kumpa zawadi mpenzi wake, haridhiki tu.Anaanza kuikosoa. Anasema haifanani na yeye, eti si ya hadhi yake. Akipewa fedha anasema hazitoshi. Kila siku ni malalamiko. Hampi nafasi mpenzi wake ya kufurahia uhusiano wao. Anamfanya kila anapokutana naye awaze atapigwa mzinga.Bahati mbaya sasa kila atakachopewa haridhiki. Anatamani kikubwa zaidi. Wanaume wengi siku hizi wanaichukia tabia hiyo. Hawapendi kuwa na mwanamke ambaye haridhiki na kile kidogo walichojaliwa. Wanaume wengi wakiona hivyo huwa wanaanza kumuepuka mwanamke wa ‘sampuli’ hiyo.Kwake kunakuwa hakuna jema. Badala ya kumshauri mpenzi wake mbinu za kujikwamua kiuchumi yeye ni lawama tu. Kila siku analalamika kwamba wanaume wengine wanawapa wapenzi wao mahitaji muhimu lakini wa kwake hamtimizii.Mwanaume akiona kila analofanya kwa mpenzi au mkewe haridhiki, hatoi shukurani ni rahisi kupunguza mapenzi kwa mtu wake. Taratibu anaanza kujitoa na hata kuhamishia mapenzi kwa mtu mwingine ambaye atakuwa anaridhika kwa kidogo anachopewa. Ni muhimu kuridhika.3. KulinganishaHii nayo ni tabia isiyopendwa na wanaume wengi. Wanaume wanapenda kuishi maisha yao. Wanapenda kuheshimiwa na wapenzi wao. Wanapenda kumsikia mwanamke akisema; ‘hakuna mwanaume mwingine wa kufanana na wewe.’Mwanaume anapenda kuhakikishiwa kwamba hakuna mwanaume mwingine kama yeye. Yeye ndiye mzuri au bora kuliko wanaume wengine hivyo mwanamke anapoanza kuonesha tabia za kumlimnganisha na mwanaume mwingine linakuwa tatizo kubwa.Mwanaume anakasirika. Anaona ni rahisi mwanamke wake kumtamani mtu mwingine baki kuliko yeye. Sifa anazozitoa kwa mwanaume mwingine ni nzuri hivyo zinamvutia. Kama zinamvutia siku yoyote anaweza kushawishika kumfuata yule anayemvutia.Wanawake wanapaswa kuwa makini katika eneo hilo. Hata kama umeona kuna kitu kizuri kimekuvutia kutoka kwa mwanaume mwingine, kamwe usije kumwambia mwenzi wako. Baki nalo moyoni. Jipe moyo kwamba mwanaume uliyenaye ndiye bora kuliko wanaume wote duniani.4. Kuwa TegemeziWakati mwingine hata kama huna kitu lakini mwanamke unashauriwa kutojionesha huna kitu. Jioneshe kwamba una kitu hata kama huna. Wanaume wa sasa hawapendi kuwa na mwanamke ambaye kila kitu anategemea kutoka kwa mwanaume.Hata kama huna kazi lakini ni vyema basi mwanamke akajaribu kufanya biashara ndogondogo ambazo zitampunguzia mwanaume wake makali ya kuombwa fedha kila wakati. Wanaume wanapenda kuwapa wapenzi wao fedha lakini inapozidi kipimo inageuka kuwa kero.Yani kuanzia mahitaji ya kila siku, saluni, mavazi, ada ya watoto na mengine mengi mwanamke anamtegemea mwanaume. Yeye hataki kujishughulisha hata kidogo. Anataka aletewe, kazi yake kubwa ni kulea familia nyumbani.Mwanaume akigundua mwanamke ni tegemezi mkiwa katika hatua za mwanzoni, ni rahisi kumkimbia mwanamke na kwenda kwa mwanamke ambaye angalau atakuwa hamtegemei kwa kila kitu. Mwanamke anayejiongeza hata kwa kutoa wazo la kuanzishiwa biashara ambayo itamfanya asiwe tegemezi.5. Kutokuwa Muelewa Mwanaume anapenda mwanamke muelewa. Hapendi mwanamke mbishi. Anatamani kuwa na mwanamke ambaye akimueleza kitu, anajiongeza na kufanya zaidi ya pale mwanaume alipofikiria. Mwanaume anapenda mwanamke atakayeanzisha wazo la kimaendeleo na kumshirikisha mpenzi wake ili walifanye.Wanaume wanapenda wanawake wanaowaelewa. Kama mwanamke anakuwa si wa kumuelewa mpenzi wake, kumsaidia basi mara nyingi mwanaume humkimbia.6. Kujigamba/Maringo Hakuna mwanaume anayependa kutawaliwa. Wanawake wenye fedha mara nyingi wanakuwa na tabia ya kutaka kuwatawala wanaume. Anataka mwanaume afanye kile ambacho yeye anataka. Fedha zinamvimbisha kichwa na kuona kwamba anaweza kuwa na mamlaka ya kumuamrisha mumewe.Anatumia fedha zake kama fimbo ya kumchapia mpenzi wake. Ni vigumu sana wanaume kumvumilia mwanamke wa aina hiyo, mara nyingi wanajiepusha naye. Kwa kutumia fedha zake anaweza kupata mwanaume mwingine lakini pia watashindwana katika suala la kumtawala.7. Kuwa bize sana Wanaume wengi hawapendi mwanamke tegemezi lakini pia wanaume haohao wanachukia mwanamke akiwa bize sana na kazi zake. Mwanaume hapendi kuona mwenzi wake anakuwa bize na kazi au biashara zake kiasi ambacho kitamfanya hata akose muda na mwenzi wake.Unachotakiwa kufanya hapo mwanamke ni kujigawa. Hakikisha unakuwa bize na kazi lakini si ya kupitiliza maana itamfanya mwanaume akose muda wa kuwa na wewe pale anapokuhitaji, badala yake anaweza kwenda kwa mwanamke mwingine ambaye hayupo bize.
Na Omary Mngindo, Kidomole.
WAKAZI wa Kijiji cha Kidomole Kata ya Fukayosi wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani wamewaomba wamiliki wa kampuni za simu kuboresha mawasiliano kwenye maeneo yao.Wakizungumza na Mwandishi wa habari kijijini hapo kwaniaba ya wenzao, Emmanuel Pantaleo na Shakila Hamisi walisema kuwa wanakabiliwa na adha ya mawasiliano, huku Pentaleo akieleza kuwa yeye anajihusisha na huduma za pesa kupitia nitandao mbalimbali, hali inayompatia changamoto kubwaPentaleo alisema kuwa mara kadhaa anapompatia mteja huduma ya kuweka au kupokea pesa kupitia mitandao hiyo analazimika kutoka ndani ya duka lake kuelekea kwenye barabara ya Bagamoyo Kiwangwa Msata ili apate mawasiliano ya kutuma au kutoa pesa."Kama ulivyoshuhudia hata wewe mwenyewe Mwandishi ulipotaka kutoa pesa, imekuchukua dakika kadhaa kufanikisha zoezi hilo sasa changamoto hii imekuwa kubwa kwa miaka mingi huku kukiwa hakuna dalili za kuondokana na adha hii," alisema Pentaleo.Kwa upande wake Shakila alisema kwamba yeye anapohitaji kupiga simu analazimika kutoka nyumbani kwake kuja maeneo ya barabarani ili kuweza kupata mawasiliano ya kupiga simu, na kwamba wakazi hao simu zao huziweka juu ya ukuta wa nyumba, inapoita wanaitafuta barabara ili wazungumze."Leo tunashukuru kutembelewa na chombo cha habari kijijini kwetu, tunaimani kwamba kilio hiki kitawafikia viongozi husika, hatimae kiweze kupata ufumbuzi, suala hili limekuwa kero kubwa sana kwa wana-Kidomole," alisema Shakila.Akizungumzia changamoto hiyo, Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mrisho Some alisema kwamba wakazi kijijini hapo sana kiu ya miaka mingi kuhusiana na adha ya mawasiliano, hivyo amewaomba wamiliki wafike waangalie namna gani wanavyoweza kupunguza kana si kumaliza adha hiyo."Kijiji chetu pekee kina wakazi 796 ambapo kati yao wanamiliki simu hivyo wanaathirika na upatikanaji wa mawasiliano, tunawaomba wamiliki au Mamlaka ya Mawasiliano TCRA wasikilize kilio hiki," alimalizia Some.