Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imetakiwa kutatua malalamiko ya upatikanaji wa baadhi ya dawa na vipimo kwa wananchi wenye bima ya afya.Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa kikao na Menejimenti ya Mfuko huo katika ofisi ndogo za wizara zilizopo jijini, Dar es Salaam.
“Kumekuwepo na malalamiko ya upatikanaji wa baadhi ya dawa na vipimo kwa watu wenye kadi za bima pia ucheleweshaji wa malipo ya watoa huduma za afya” Alisema Waziri Ummy.Aidha, Waziri Ummy ameutaka mfuko huo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko huo pamoja na mafao yanayotolewa katika vifurushi vya bima ya afya.“Tatueni malalamiko yote kwa wakati ili wananchi wafurahie vifurushi vyote watakavyojiunga navyo”.Alisisitiza Waziri Ummy.
Kikao hicho pia kiliangalia mwenendo wa utoaji wa huduma za bima za afya zinazotolewa na mfuko huo ambapo kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NHIF, Benard Konga, Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, na Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi Tirioni 11.4 baada ya kushinda mashauri mbalimbali yaliyoendeshwa katika Mahakama mbalimbali ndani na nje ya nchi.Hayo yamezungumzwa mapema leo na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Mhe. Gabriel Malata alipokuwa akipokea msaada wa kompyuta mpakato tano zenye thamani ya shilingi milioni 7.5 zilizotolewa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Mhe. Malata ameeleza kuwa kiasi hicho cha fedha kimeokolewa katika mwaka wa fedha 2019/2020 kufuatia utendaji mzuri wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ambao umepelekea kushinda mashauri mengi yaliyofunguliwa dhidi ya Serikali.Kiongozi huyo aliongeza kuwa fedha hizo zilizookolewa na Serikali zitasaidia katika kuboresha miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kama vile ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), ununuzi wa ndege na meli kubwa za abiria na mizigo katika kuhakikisha tunafikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.Amesema kuwa kompyuta hizo zimekuja muda muafaka kwani zitawawezesha watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu Mkuu wa Serikali kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kwa haraka zaidi hatua itakayosaidia kuongeza ufanisi zaidi katika majukumu yao.Aidha, Naibu Wakili Mkuu ameongeza kuwa kompyuta hizo zitakuwa msaada mkubwa kwa Ofisi yake kwa kuzingatia ukweli kuwa mwaka huu tunaenda kwenye zoezi la uchaguzi hivyo itawawezesha watumishi wake hususani mawakili katika kutekeleza majukumu ya usimamizi wa mashauri.“Mwaka huu tuna jukumu la uchaguzi na uchaguzi huwa unapelekea kuibuka kwa mashauri mengi yanayofunguliwa kwa ajili ya kupinga matokeo ya uchaguzi”, alisema Mhe. Malata.Naye Bw. Muungano Saguya ambaye ni Meneja Huduma kwa Jamii katika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) alisema kuwa wameamua kutoa msaada huo ili kuwasaidia watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha zaidi hatua itakayopelekea kuendelea kuokoa fedha nyingi ambazo zingeweza kupotea kutokana na upungufu wa vitendea kazi ofisini hapa.Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ilianzishwa feburuari 12 mwaka 2018 kwa tangazo la serikali Na. 50 ikiwa na lengo la kuratibu, kusimamia na kuendesha mashauri yote ya madai pamoja na Katiba, Uchaguzi na haki za binadamu yanayofunguliwa dhidi ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Beki wa Liverpool Joel Matip baada ya kufanyiwa vipimo vya kina sasa imethibitika atakosa game zote za Liverpool zilizosalia 2019/20, Matip aliumia mguu wakati wa game ya Liverpool dhidi ya Everton.
CAF watangaza kuwa sababu ya Corona michuano ya AFCON 2021 iliyokuwa ifanyike Cameroon sasa imesogezwa mbele hadi January 2022.
Na Amiri Kilagalila, Njombe.
Wasaidizi wa kisheria nchini wameelezwa kuzingatia maadili katika utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wahitaji ili waweze kupata nafuu na haki inayohitajika kwa mujibu wa sheri.Wito umetolewa na katibu mkuu wa wizara ya katiba na sheria Prof.Sifuni Mchome wakati akizindua kamati ya uratibu wa shughuli za msaada wa kisheria mkoa wa Njombe.
“Katika kazi ni wajibu kuhakikisha maadili yanazingatiwa,maadili katika maeneo mbali mbali,maadili katika ushauri,kupeleka kesi mahakamani na maadili katika mahusiano yetu na watu ambao tunawahudumia,na mtoa msaada wa kisheria hawezia akawa mchonganishi”alisema Prof.Sifuni MchomeAidha Mchome amesema lengo mojawapo la serikali kuwa na wasaidizi wa msaada wa kisheria ni kusaidia katika utetuzi wa migogoro inayojitokeza katika jamii pamoja na kuhakikisha uwepo wa utawala bora.
Naye mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka ameiomba wizara ya katiba na sheria kuongeza nguvu katika kuzisimamia asasi zinazotoa elimu kutokana na uwepo wa asasai zinazofanya kazi isiyokuwa na afya kwa taifa.“Kwa muda mrefu huko nyuma asasi hizi zingine zilikuwa zikifanya kazi ambazo hazina afya kwa ustawi wa nchi na wengine wamekuwa ni madalali wa kusimamia maslai ya nchi zingine za ughaibuni”alisema Ole SendekaKaimu aifisa maendeleo ya jamii mkoa wa Njombe Farahani Kanyenda,amesema wasaidizi na watoa huduma za msaada wa kisheria wamekuwa na msaada mkubwa kwa jamii na kuwezesha idadi ya watu waliopata huduma ya msaada wa kisheria kwa kipindi cha Julai 2019 hadi Mei 20 kufika 8282 kwa upande wa madai,19 kwa upande wa Jinai,26 kwa upande wa matunzo huku watoto waliopata msaada wa kisheria wakiwa 42.Erasto Mkiwa ni mratibu wa shirika la PAD na Geofrey Kaduma ni mkurugenzi wa kituo cha msaada wa sheria Njombe,wanasema licha ya uwepo wa changamoto katika shughuli zao lakini wanaamini kamati iliyoundwa itasaidia kuwafikia zaidi wananchi wenye migogoro mbali mbali.“Kwa kupitia kamati hii itatusaidi kuwafikia zaidi wananchi kwasababu ni sehemu mojawapo ya kurahisisha mawasiliano na kupitia wadau tuliopo ni rahisi kuelewa wapi kuna tatizo”Alisema Erasto Mkiwa
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuwafukuza kazi wafanyakazi wa shirika hilo wanaowatoza fedha na wanaochelewesha zoezi Kutoa nembo ya ubora kwa bidhaa zinazotengenezwa kwenye Viwanda vidogo nchini.Waziri Bashungwa ametoa maelekezo hayo leo 30 juni 2020 alipofanya ziara mkoani Simiyu na kutembelea kiwanda cha Usindikani wa Viazi lishe kilichopo wilaya ya Maswa kinachojulikana kwa jina la Ng’hami Industries Company Ltd.
Bashungwa amefikia maamuzi hayo baada ya kufika kiwandani hapo na kukagua bidhaa za kiwanda hicho ambayo ni unga wa viazi lishe na kugundua hazina nembo ya ubora ya TBS, ambayo changamoto hiyo imesababiswa na wafanyakazi wa shirika la TBS kwa kuwaomba fedha kwa ajiri ya kupewa nembo ya ubora pia kuchewesha kwa zaidi ya miezi saba bila kupewa majibu au nembo ya ubora.Waziri Bashungwa baada ya kuona changamoto hiyo alimpigia simu Mkurugenzi Mkuu wa TBS na DKt. Yusuph Ngenya na kumuelekeza kuwafukuza kazi wafanyakazi wake wanaokwenda kinyume na maagizo ambayo amekuwa akiyatoa mara kwa mara ya kutowachelewesha wafanyabiasha kwa sababu ambazo sio za msingi zinazosababisha bidhaa kutopewa nembo za ubora kwa wakati ambazo zinasababisha mazingira ya Rushwa na usumbufu kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali.Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho Bw. Ntobi Rufunga ameeleza kuwa barua ya kuomba nembo ya ubora ilipelekwa TBS tangu mwezi 11, 2019 lakini mpaka sasa hajapewa majibu yoyote na baada ya kuchukuliwa kwa sampuli ya bidhaa hiyo wameombwa kutoa kiasi cha Tsh. 520,000/= ili wapewe nembo ya ubora ambayo ni kinyume na sheria na mashariti ya shirika hilo.Aidha Bw. Ntobi amesema kuwa Kiwanda hicho mpaka sasa kinazalisha unga wa viazi lishe wa aina mbili ambao ni Unga wa kupika uji kwa ajiri ya matumizi ya rika zote pia Unga wa kutengeneza keki, mikate na andazi.
Yanga yafanikiwa kutinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) baada ya kuipiga Kagera Sugar bao 2-1 katika dimba la Taifa jijini Dar Salaam.Magoli ya Yanga yalifungwa na Molinga dakika ya 52, Kaseke dakika ya 76 kwa mkwaju wa penati na lile la Kagera lilifungwa na Awesu dakika ya 20.
FT: Yanga SC 2-1 Kagera Sugar.